
Kifaa cha umeme kinachopandikizwa ambacho huwekwa kwenye fuvu na waya wake kuwekwa kwenye ubongo ninaweza kutambua na kutobi msongo mkubwa wa mawazo, wanasayansi wa Marekani wananaamini baada ya matokeo mazuri kupatikana kwa mgonjwa wa kwanza.
Sarah, mwenye umri wa miaka 36, alikuwa na kifaahicho alichowekewa kwenye fuvu kwa zaidi ya mwaka mmoja uliopita na anasema kimebadilisha kabisa maisha yake.
Kifaa hicho chenye ukubwa wa boksi la vibiriti kimekuwa wakati wote kichwani kwake "kikiwaka" lakini kikifanya kazi tu pale kilipohisi huenda anahitaji huduma yake.
Utafiti wa majaribio unaelezewa katika jarida la masuala ya tiba la Nature Medicine journa
Watafiti kutoka Chuo kikuu cha California, San Francisco, wanasisitiza kuwa ni mapema sana kusema iwapo kinaweza kuwasaidia wagonjwa wengine, kama Sarah, wenye msongo wa mawazo mgumu kuutibu, lakini wanamatumaini na wanapanga kufanya majaribio zaidi
Mtafiti dokta Katherine Scangos, ambaye ni daktari wa magonjwa ya akili katika chuo kikuu, alisema kuwa uvumbuzi huo uliwezekana kwa kubaini "mizunguko ya msongo wa mawazo" katika ubongo wa Sarah.
"Tulibaini eneo moja, ambalo ni eneo linaloitwa ventral striatum, ambako vichocheo mara kwa mara vimekuwa vikiondoa hisia zake za msongo.
"Na pia tulibaini eneo la shuguli za ubongo kwenye amygdala ambalo linaweza kubashiri wakati hali yake ilikuwa mbaya zaidi."
Wanasayansi wanasema mengi yanahitajika kupima jaribio la tiba hiyo na kuamua iwapo inaweza kuwasaidia watu zaidi wenye msongo mkubwa wa mawazo, na labda hali nyingine pia za kiafya.
No comments:
Post a Comment