Search This Blog

Friday, October 15, 2021

Mpenzi wake Agnes Tirop akamatwa akitoroka


Maafisa wa polisi nchini Kenya wamemkamata mume wa mwanariadha anayeshikilia rekodi ya dunia katika mbio ndefu Agnes Tirop ambaye alidungwa kisu hadi kufa nyumbani kwake.

Emmanuel Rotich , ambaye alikamatwa katika mji wa pwani ya Kenya Mombasa , atakabiliwa na mashtaka uchunguzi utakapokamilika , afisa alisema.

Bi Tirop mwenye umri wa miaka 25 alipatikana amefariki siku ya Jumatano katika mji wa magharibi wa Iten , kituo cha mazoezi cha wanariadha.

Alikuwa amemaliza wa nne katika mashindano ya mwaka huu ya Olimpiki mjini Tokyo katika fainali ya mbio za mita 5000.

Mwaka 2019, alishinda medali ya shaba katika mbio za mita 10,000 katika mashindano ya ubingwa ya dunia.

Mume wake kwasasa anazuiliwa baada ya kukamatwa alipokuwa akitoroka, kwa mujibu wa George Kinoti , mkurugenzi wa idara ya jinai , akizungumza na kitengo cha habari cha AFP.

Salamu za rambirambi zimetolewa na raia wengi wa Kenya pamoja na wanariadha wenzake.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...