Search This Blog

Friday, October 15, 2021

Wanawake watano kutoka DRC waishtaki Ubelgiji kwa kuwatenganisha na wazazi wao kwa lazima


Wanawake watano wenye asili ya Kongo na Ubelgiji, waliotengwa na familia zao wakati wa ukoloni wameishtaki serikali ya Ubelgiji kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu.

Wanawake hao wanasema walichukuliwa kutoka kwa mama zao weusi wakati wa kuzaliwa tu kwa msingi wa rangi ya ngozi yao.

Wanawake hao watano walikuwa kati ya maelfu ya watoto waliochukuliwa kutoka kwa familia zao na kupelekwa kituo cha kulelea watoto cha kidini kwa kuwa lilikuwa ni agizo kwa wakati ule wa ukoloni.

Wengi wao walikuwa hata hawawafahamu baba zao wazungu. Wale ambao wameenda mahakamani hawakuletwa Ubelgiji wakati Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo ilipopata uhuru mnamo 1960.

Ubelgiji inashtakiwa kwa uhalifu dhidi ya ubinadamu, kosa ambalo hakuna kikomo cha wakati.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...