Search This Blog

Saturday, October 2, 2021

Merkel ataka mamluki waondoke Libya


Kansela Angela Merkel wa Ujerumani ametota wito wa kuondolewa mamluki wote nchini Libya. Bibi Merkel alitoa wito huo mjini Berlin kwenye mkutano na rais wa kipindi cha mpito wa Libya, Mohammed Minfi, anayefanya ziara nchini Ujerumani. 
 
Kansela Angela Merkel amesema mustakabali wa Libya unapaswa kujengwa na watu wa Libya bila ya ushawishi kutoka nje. Merkel pia amesisitiza umuhimu wa uchaguzi uliopangwa kufanyika mwezi Desemba na ameahidi kuwa Libya itaendelea kupewa kipaumbele katika sera ya nje ya Ujerumani. 
 
Kwenye mkutano wao huo, kiongozi wa Ujerumani pia ameahidi kuiunga mkono Libya kiuchumi. Ujerumani ni miongoni mwa nchi zinazosuluhisha katika mgogoro wa nchi hiyo ya Afrika Kaskazini.    

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...