Majimbo kadhaa ya Ujerumani yanaondoa vizuizi vilivyosalia vya kupambana na maambukizo ya virusi vya corona.
Hata hivyo, bado maafisa wana wasiwasi na athari za janga hilo na wamewataka raia kuendelea kujilinda, wakisema maambukizo mapya yapo lakini kwa kiwango cha chini. Katika jimbo lenye idadi kubwa ya wakaazi kuliko mengine yote nchini Ujerumani la North Rhine-Westphalia, watu hawatalazimishwa kuendelea kuvaa barakoa katika maeneo ya wazi ingawa bado wanashauriwa kufanya hivyo.
Ukomo wa idadi ya watu wanaoruhusiwa kutazama mechi za mpira viwanjani na katika matamasha pia utaondolewa. Katika jimbo la Bavaria vilabu, kumbi za disko na sehemu nyingine za burudani zitafunguliwa tena baada ya kufungwa kwa mwaka mmoja na nusu.
No comments:
Post a Comment