Na Timothy Itembe Mara.
Mbunge wa jimbo la Tarime Mjini Michael Kembaki amepongeza serikali awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassani kwa kuipatia halmashauri ya Mji wa Tarime shilingi bilioni Tatu kwaajili ya ujenzi wa soko.
Mbunge huyo alisema kitendo cha Serikali kuipatia halmashauri shilingi bilioni Tatu kwa ujenzi wa soko kama pesa ya kuanzia mradi kimerudisha imani ya Chama cha mapinduzi kwa wafanyabiashara waliokuwa wamekata tamaa huku wakiangaika wakitafuta maeneo ya kufanyia biashara zao.
Kembaki alitumia nafasi hiyo kuwaomba wanatarime kuendelea kutoa ushirikiano kwa Chama chake ili kuleta maendeleo na changamoto mbalimbali kupungua ikiwemo ya ukosefu wa maeneo ya kufanyia biashara.
Akizungumza kwenye mkutano wa hadhara uliofanyikia viwanja vya Sabasaba kaimu mkurugenzi,Praiton Garigo alisema serikali imeleta shilingi bilioni Tatu za mradi wa ujenzi wa soko kuu ambalo awali lilibomolewa na kuwa mradi huo upo mbioni kuanza na wafanyabiashara wakanufaika.
Soko hilo lilibomolewa mwaka jana baada ya halmashauri kudai kuwa linatakiwa kujengwa soko la kisasa na mji kuwa na hadhi tofauti na ulivyokuwa na majengo yamechakaa na kuleta sura tofauti inayoonyesha uchakavu.
Kwa upande wa mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Tarime,Daniel Komote alisema bajeti ya ujenzi wa soko hilo ni zaidi ya shilingi bilioni 8 na kuwa serikali imeleta shilingi bilioni 3 za kuanzia mradi hatimaye zilizobaki zitatolewa kwa awamu.
Emanuel Buchafye alisema kuwepo na uwiano wa kugawa vibanda na vizimba kwa kuzingatia wafanyabiashara waliobomolewa awali na sio vinginevyo.
Buchafye aliongeza kuwa kusiwepo utiritimba wa kugawa vibanda na vizimba huku wakapewa na kugawiwa kwa upendeleo wafanyabiashara ambao ni wageni na wasio wa awali waliokuwepo.
Kufanya hivyo kutaondoa mgogoro utakao weza kujitokeza katika swala zima la kugawa vibanda na vizimba ndani ya soko hilo kwa hali hiyo waungane katika kutenda haki.
No comments:
Post a Comment