Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Wafugaji wameshauriwa kufuata kanuni bora za ufugaji wa mifugo yao ili waweze kunufaika na kubadirisha mfumo wa maisha yao.
Hayo yamesemwa na Dkt.Heriel Massawe kutoka Taasisi ya Utafiti wa mifugo Tanzania (TARIRI) Mabuki Mkoani Mwanza alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari walipomtembelea kwa lengo la kujifunza maswala ya Tafiti za kisayansi na tekinolojia.
"Sisi tunashughulika na Utafiti wa mifugo kama Ng'ombe,mbuzi tunatoa huduma kwa jamii inayotuzunguka tunafanya kuzalisha pamoja na uboreshaji wa Ng'ombe asili na madume ya ankole na mpaka sasa kuna ndama mia 400 zimezaliwa kwa wafugaji na mbuzi pia zimezalishwa kutoka Wilaya ya Kwimba na tunawauzia wafugaji madume ambayo yataleta tija kwao igawa majike siyo mengi kwahiyo kufuata Utafiti huu wa kuchanganya mbegu za asili na za kutoka Nchini jirani tunapata nyama tamu kama wengi wananvyosema kuwa mbengu ya ankole kutoka Uganda ni tamu kwa mfugaji akielewa vizuri atapata faida kubwa Sana amesema Massawe.
Amesema mfugaji akifuata kanuni na akiweka jitihada binafsi atanufaika na akiachana na ufugaji holela lakini pia wakisikia kuna sehemu ya mafunzo wajitokeze na ofisi zetu ziko wazi wazitumie ili wanufaike kupitia Utafiti wa kupandikiza mbegu hizi na tumebaini malisho bado siyo rafiki tumeamua kuchukua mbegu za majani na kuzifanyia Utafiti ambazo zinavulimia mazingira ya aina yoyote ile ili tuweze kumkomboa mfugaji kutokata tamaa kisa kukosa majani ya kuisha mifugo yake kuna majani yanatokea Nchini Brazil ambayo yanavumilia ukame kwahiyo kwa mfugaji ambae anahitaji afike hapa ofisini kwetu tuweze kumwelekeza ili mifugo yake isikose chakula na kusababisha hasara kwake na kwakuwa na sisi tunapata ufadhili kutoka Taasisi ya Costech inatufadhili katika Utafiti wetu ni lazima tujikite zaidi kwa walaji ambao ni wananchi ilu waweze kunufaika na Tafiti ambazo tunafanya na lazima tujitahidi kufanya kazi ili jamii ipate uwelewa zaidi.
James Manjala kutoka Kijiji cha Mabuki Mkoani Mwanza ni mmoja wa wafugaji wa Ng'ombe aliyenufaika na Utafiti wa kupandikiza dume za ankole amesema kabla ya kupata ujuzi huo kutoka kwa watafiti alikuwa akiuza Ng'ombe mmoja kwa shilingi laki 150,000 hadi 200,000 ila alivyopata elimu ya kupandikiza mbegu hiyo anauza Ng'ombe mmoja kwa laki 700,000 hadi 500,000 ameweza kubadirisha mfumo wa maisha yake kwa kuzingatia elimu kutoka kwa watafiti wa mifugo pamoja na kanuniwalizomuelekeza.
"Kiukweli ilifikia muda sisi kama familia tulikuwa tunafuga ijimradi watu wasituseme maana tulikuwa tunatumia nguvu nyingi mavuno kidogo ila tokea hawa watafiti walivyo tupatia elimu ya kupandikiza hii mbegu ya ankole kutoka Uganda tunafurahia ufugaji na mabadiriko yapo makubwa kwahiyo nawashauri wananchi kufuatilia mambo ya watafiti na kuzingatia elimu wanazotoa kuna faida kubwa mno jamani amesema Manjala.
Mbali na kuzungumza na Mtafiti na mnufaika tukaamua kwenda hadi chuo cha Dar es salaam institute college (DIT)tumekutana na Mwalimu Leonard Mayunga ambae ni mtaalamu wa utengenezaji wa bidhaa za ngozi Mkoani hapa kwa lengo la kutaka kufahamu upatikanaji wa ngozi na ubora wake amesema kuwa,wataalamu wa ngozi bado wanahitajika Nchini Tanzania kwani bado ni fursa ambayo iko wazi na inalipa.
Ramadhani Khalfan ni mtaalamu wa utengenezaji wa bidhaa za ngozi kutoka chuoni hapo amesema kuwa kuna baadhi ya ngozi ambazo tunakutana nazo zinakuwa hazina ubora unakuta ngozi inamichirizi na tatizo linaanzia kwa mfugaji kutokuwa na matunzo mazuri na upatikanaji wa ngozi kuna muda unakuwa ni shida kama mfugaji akifuata kanuni zote ananufaika mara mbili kupitia nyama na ngozi kwahiyo wafugaji wafuate kanuni na wawatumie wataalamu kwa faida yao amesema Ramadhani.
"Wakazi wa Mwanza naona hawajatambua fursa iliyowazunguka ya ubunifu wa kutumia ngozi na labda nitoe wito kwa wanyeji wa Mwanza na kanda ya ziwa wajitokeze kujifunza na uhakika wa ajira upo siyo lazima uwajiliwe ni fursa ambayo haina longolongo wake DIT wajifunze kutumia bidhaa za ngozi amesema Ramadhani.
Wanafunzi waliohitimu mafunzo ya utengenezaji wa bidhaa za ngozi chuoni hapo Jacob Machage na Cecilia Dominiko wameiomba Serikali kuwasaidia vijana wenye ujuzi kwa kuwapatia vifaa ambavyo vitaweza kurahisisha utendaji kazii wao kuliko kukaa nyumbani na kuwa tegemezi katika familia.
Miongoni mwa wanufaika na mafunzo kutoka chuo cha DIT ni kikundi cha Umoja Leather Ilemela muweka hazina wa kikundi hicho Emmanuel Malando amesema wamenufaika na mafunzo ya kutumia bidhaa za ngozi wanatengeneza viatu aina mbalimbali zenye ubora mzuri amewaomba Watanzania kuamini bidhaa zinazotengenezwa Nchi.
Malando amesema changamoto waliyonayo ni ukosefu wa mtaji kwani bado hawajaimarika kiuchumi kutokana na mahitaji ya kutengenezea bidhaa kuwa na bei kubwa na kusababisha baadhi ya wananchama kukata tamaa na kuniondoa kwenye kikundi.
Naye Dkt.Philber Luhunga mkurugenzi wa menejimenti ya maarifa Tume ya Taifa ya Sayansi na tekinolojia (COSTECH) amesema tekinolojia zote nilazima ziwafikie wananchi ili waweze kunufaika ilu waweze kuzitumia kwa lengo la kubadirisha maisha yao na kukuza uchumi kupitia tekinolojia za kisayansi kwani Serikali imewekeza sana katika kilimo maana asilimia kubwa ya Watanzania wanategemea kilimo.
Luhunga amesema anawatengemea waandishi wa habari kutangaza Tafiti za kisayansi na tekinolojia kwa wananchi ili waweze kunufaika kwani wao ndio walaji wakubwa wa Tafiti mbalimbali zinazofanywa na watafiti aliyasema hayo wakati wa kuhitimisha ziara ya waandishi wa habari na watafiti Wilaya I Sengerema Mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment