Search This Blog

Monday, October 4, 2021

Mazungumzo ya kuunda serikali ya mseto Ujerumani yaendelea


Vyama vya SPD na FDP vimekutana kwa mazungumzo ya kwanza mjini Berlin kujadili uwezekano wa kuunda serikali ya mseto. 
 
Baada ya hapo, chama cha SPD pia kilifanya mazungumzo na chama cha Kijani. Hali kadhalika muungano wa vyama vya kihafidhina vya CDU/CSU ulifanya mazungumzo na chama cha FDP. 
 
Kimahesabu, kufuatia uchaguzi wa mwezi uliopita, kuna uwezekano wa kuundwa serikali inayoongozwa na SPD au muungano wa CDU/CSU. Lakini kwa vyovyote vile, vyama vya FDP na Kijani vitahitajika kuunda serikali ya mseto.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...