Search This Blog

Monday, October 4, 2021

Kibu Denis ni mtanzania, ruksa kukipiga Simba SC


Klabu ya Simba SC imethibitisha kuwa nyota wake Kibu Denis amemaliza utata wa uraia wake na sasa ameruhusiwa kuichezea klabu hiyo pamoja na timu ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars ).

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Simba SC ambayo imemsajili Kibu Denis katika dirisha kubwa la usajili kabla ya kuanza msimu huu akitokea Mbeya City imethibitisha kumaliza sakata hilo.

Kabla ya kujiunga na Simba SC, Kibu Denis ameshawahi kucheza katika madaraja mbalimbali ya soka nchini ikiwa Ligi daraja la tatu, Daraja la kwanza na ligi kuu.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...