
Uuzaji wa mali ya jambazi maarufu wa Marekani Al Capone umekusanya jumla ya dola milioni tatu za kimarekani (£ 2.2m) kwenye mnada uliofanyika mwishoni mwa wiki huko California.
Baadhi ya vitu 174 - pamoja na silaha za moto na picha za kibinafsi pamoja na vito na samani- zimeonyeshwa.
Hafla hiyo, inayoitwa Karne ya Umaarufu: Mali ya Al Capone, ilifanyika katika kilabu cha kibinafsi na ilivutia wazabuni karibu 1,000.
Bidhaa maarufu zaidi ilikuwa bunduki inayopendwa na Capone, ambayo iliuzwa kwa $ 860,000.
Bunduki hii inaaminika ilkuwa bei ya juu zaidi ya silaha ya karne ya 20 iliyouzwa kwenye mnada, kulingana na Chicago Tribune.
Al Capone alikuwa mhalifu mkubwa Chicago aliyejulikana kama Adui Namba moja wa Umma kwa utawala wake mfupi kama kiongozi wa uhalifu miaka ya 1920.
No comments:
Post a Comment