Wanajeshi na polisi wamepelekwa katika shule zote katika Eswatini ambako wanafunzi wamekuwa wakifanya maandamano kwa wiki kudai mageruzi ya kisiasa.
Shule za msingi na sekondari katika nchi hiyo pekee ya Kiafrika inayotawaliwa Kifalme zamani ikifahamika kama Swaziland, wamekuwa wakisusia kuingia madarasani na kufanya mgomo baridi kwa mwezi mzima uliopita.
Hapo nyuma, maandamano ya wanaounga mkono demokrasia yalikuwa yakifanyika katika maeneo ya mijini, lakini katika kipindi cha mwaka hvijijini-ambako maandamano hayo yamekuwa yakionekana miongoni mwa jamii za vijijini-ambako kwa kawaida wamekuwa walimuunga mkono Mfalme.
Maafisa wa usalama wamekuwa wakionekana katika miji mikuu ya Eswatini-Mbabane na Manzini.
Maafisa wanasema wamepelekwa kusaidia kuimarisha amani lakini wanafunzi waandamanaji wanaamini ni kuwatisha.
Maandamano ya wanafunzi ya wiki hii ni ya hivi karibuni katika miezi ya hivi karibuni ya ghasiakatika ufalme huo mdogo.
Wanatoa wito wa hali bora za kusoma na elibu ya bure. Wanasema garama ya elimu katika shule za taifa haipatikani kwa wengi-katika nchi ambako karibu 25% ya watu wazima hawana ajira.
Waandamanaji, ambao wamekuwa wakikusanywa na makundi ya wanafunzi, pia wanadai kuachiliwa kwa wabunge wawili waliokamatwa wakati wa maandamano ya kudai demokrasia mapema mwaka huu.
Mfalme Mswati IIIaliwahi kuwashutumiwa na wanaharakati kwa kutumia ghasia kuwanyamazisha wapinzani wake wa kisiasa-baadhi wanaona kusambazwa kwa wanajeshi kama sehemu ya kutekeleza nia hiyo.
Ufalme wa Eswatini ni mojawapo ya nchi masikini zadi barani Afrika-walosoaji wake wanamshutumu kwa kuishi maisha ya anasa huku watu wake wakikabiliwa na njaa kila siku.
Wachambuzi wa siasa wanasema maandamano ya mara kwa mara ya upinzani ni ishara ya kutaka mabadiliko nchini-kwamba watu wanaendelea kutofurahia utawala uliopo sasa madarakani.
No comments:
Post a Comment