Polisi nchini Jamuhuri ya Kidemkrasia ya Congo wamefyatua vitoa machozi wakati wanaharakati wa chama tawala walipojaribu kuwazuia maelfu ya wanachama wa upinzani walioandamana wakidai tume huru ya uchaguzi.
Waandamanaji wa upinzani waliangusha sanamu ya rais Felix Tshisekedi pamoja na bendera ya chama chake cha Union for Democracy and Social Progress UDPS.
Wanachama wa UDPS walijaribu kuwazuia waandamanaji na polisi wakayatua vitoa machozi ili kuwatawanya kuruhusu maandamano kuendelea.
Maandamano hayo yaliongozwa na Martin Fayulu, mgombea wa urais mwaka 2018 pamoja na aliyekuwa waziri mkuu Adolphe Muzito.
Fayulu ameshtumu utawala wa Tshisekedi akidai kwamba umesababisha umaskini na njaa kwa sababu ya kile alichokitaja kama kujighubika kwenye ufisadi.
No comments:
Post a Comment