Search This Blog

Sunday, October 17, 2021

Maelfu ya watu waandamana Sudan kupinga serikali

 


Maelfu ya waandamanaji wanaounga mkono jeshi, nchini Sudan wamejitokeza mitaani kushinikiza kuvunjwa kwa serikali ya mpito kwa madai kwamba "imefeli " kisiasa na kiuchumi. 

Haya yamejiri wakati kuna mpasuko wa kisiasa Sudan kati ya vikundi vinavyoongoza mchakato wa mpito unaokumbwa na msukosuko, baada ya miongo miwili ya utawala wa mkono wa chuma wa rais wa zamani Omar al-Bashir, aliyeng'olewa madarakani na jeshi Aprili 2019. 

Maandamano hayo yameandaliwa na kundi lililogawika kutoka vuguvugu liitwalo Forces for Freedom and Change, FCC, ambalo lilihusika pakubwa kuandaa maandamano dhidi ya Bashir na pia kuwa mshirika mkubwa kwenye mchakato wa mpito. 

Waandamanaji wameishtumu serikali ya sasa kwa kushindwa kuleta haki na usawa na wanataka serikali itakayoongozwa na jeshi.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...