Search This Blog

Sunday, October 17, 2021

Rais Macron ametaja mauwaji ya Waalgeria kuwa "uhalifu usiosameheka"

 


Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekashifu ukandamizaji dhidi ya waandamanaji wa Algeria uliofanywa na polisi mjini Paris miaka 60 iliyopita. 

Macron ametaja tukio hilo kama "uhalifu usiosameheka.

" Hii ni mara ya kwanza kwa rais wa Ufaransa kutambua mauwaji hayo ambapo miili mingi ya Waalgeria ilitupwa kwenye mto Seine. Oktoba 17 mwaka 1961 chini ya amri ya mkuu wa polisi wa wakati huo Maurice Papon, polisi iliwashambulia waandamanaji 25,000 wa chama cha FLN wa Algeria waliopinga amri ya kutotoka nje iliyowekwa dhidi yao. 

Macro alihudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya mauwaji hayo jana Jumamosi katika daraja la Bezons Magharibi mwa Ufaransa, mahali ambapo maandamano hayo yalianza na miili mingi ilipatikana kutoka mto Seine. 

Kwa muda mrefu Ufaransa ilificha au ilikataa kutambua mauwaji hayo yaliyofanyika wakati wa vita dhidi ya utawala wake nchini Algeria. 

Idadi kamili ya waliowawa katika vita hivyo haikujulikani lakini baadhi ya wanahistoria wamedai zaidi ya watu 200 waliuwawa.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...