Raia wa Haiti anayejitambulisha kuwa kiongozi wa genge lililowateka nyara wamishionari wa Kimarekani na Canada ametuma ujumbe wa video kupitia mtandao wa YouTube, akitishia kuwauwa mateka wake, endapo hakupata anachokitaka.
Msemaji kwenye video hiyo ametambuliwa nchini Haiti kama Lamo Sanjou, kiongozi wa genge liitwalo Mawozo 400, ambalo mamlaka nchini humo linasema linahusika na utekaji nyara huo uliofanyika mwishoni mwa wiki.
Wamishionari hao 16 wa Kimarekani na mmoja wa Canada, wakiwemo watoto watano, walikuwa kwenye ziara iliyoandaliwa na Jumuiya ya Misaada ya Makanisa yenye makao yake Ohio, Marekani.
Waziri wa Sheria wa Haiti, Liszt Quitel, amesema watekaji nyara wamedai dola milioni moja kama kikomboleo cha kila mmoja kati ya mateka wao. Jana, Alkhamis, Ikulu ya Marekani ilisema ingelifanya kila iwezalo kuwaokowa mateka hao.
No comments:
Post a Comment