Wabunge nchini Benin wamepiga kura kuhalalisha utoaji mimba na kuongeza wigo wa jambo hilo ambalo tayari lilikuwa likifanyika.
Wanawake sasa wanaweza kutoa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito iwapo kama ujauzito huo utamsababishia shida katika masuala ya elimu, kazi, maadili au mtoto anaweza kuathiri maisha ya mama au kwa ajili ya maslahi ya mtoto.
Kabla, utoaji mimba ulikuwa unaruhusiwa kisheria endapo mwanamke alibakwa au maisha ya mama yalikuwa hatarini kwasababu ya ujauzito.
Benin ilikuwa inaruhusu utoaji mimba kama afya ya mtoto ambaye hajazaliwa itaathirika.
Sheria mpya , ilipitishwa Jumatano usiku baada ya majadiliano makali bungeni , lakini bado katiba inapaswa kupitishwa mahakamani kabla ya utekelezaji kuanza.
Waziri wa afya Benjamin Hounkpatin ameunga mkono sheria mpya hiyo na kusema itaweza kuleta haueni kwa wanawake wengi ambao wanapata ujauzito wasioutaka na hivyo kutafuta njia hatari zinazohatarisha maisha yao ili kutoa mimba.
"Nchini Benin, karibu wanawake 200 wanakufa kila mwaka baada ya kupata matatizo wakati wa kutoa ujauzito ," alisema.
No comments:
Post a Comment