Search This Blog

Friday, October 22, 2021

Kiongozi wa Wakristo aitwa kwa mahojiano Lebanon


Mkuu wa Jeshi la Wakristo nchini Lebanon, Samir Geagea, ameitwa kwa mahojiano kufutia ghasia zilizozuka kwenye maandamano ya Waislamu wa madhehebu ya Shia wiki iliyopita, ambapo watu saba waliuawa. 
 
Afisa mmoja wa mahakama ameliambia shirika la habari la AFP kwamba idara ya ujasusi ya jeshi la taifa imeagizwa kumuhoji Geagea kutokana na maelezo yaliyotolewa na wanachama wa kundi lake waliokamatwa baada ya ghasia hizo. 
 
Maandamano ya tarehe 14 Oktoba yaliitishwa na makundi ya Kishia ya Amal na Hizbullah kudai kujiuzulu kwa Jaji Tarek Bitar, anayeongoza uchunguzi wa mripuko wa mwaka 2020 katika bandari ya Beirut.
 
Amal na Hizbullah wanalituhumu jeshi hilo liitwalo kwa kifupi cha Lebanon Forces, linalomuunga mkono Jaji Bitar, kuhusika na mauaji ya waandamanaji wao. Duru za masuala ya usalama nchini Lebanon zinahofia viashiria vya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...