Search This Blog

Friday, October 8, 2021

Huenda Nato ikaunga mkono Sahel – Mkuu wa Umoja wa mataifa asema


Muungano wa Nato unaangalia uwezekano wa kutoa usaidizi kwa vikosi vinavyopigana dhidi ya makundi ya Jihad katika jimbo la Sahel, amesema katibu mkuu wa Umoaja wa Mataifa António Guterres katika barua iliyoripotiwa na shirika la habari laAFP.

Alisema kuwa hatua hiyo "ni njia yenye ufanisi zaidi ya kutoa usaidizi wa kudumu na wa kuaminika kwa kikosicha pamoja ".

Kuna takriban wanajeshi 5,000 katika kanda ya Sahelkutoka nchi za Mali, Mauritania, Niger, Chad na Burkina Faso.

Marekani hadi sasa imekataa mpango ambao ulikuwa umeungwa mkono Ufaransa nan chi nyingine za Afrika, AFP imeripoti.

Umoja wa Mataifa unatoa wito wa kuwepo usaidizi zaidiwa kimataifa kwa vikosi katika kanda ya Sahel.

Makundi ya Jihad yamekuwa yakiendesha mashambulio katika nchi za Sahel wakiwalenga raia na wanajeshi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...