Wasafiri kutoka Tanzania ,Kenya na Uganda ni miongoni mwa watakaoruhusiwa kuingia Uingereza kuanzia jumatatu iwapo wamepokea chanjo kamili .

Serikali ya Uingereza imeyaondoa mataifa 54 kutoka orodha yan chi ambazo raia wake walihitajika kujitenga katika karantini kwa muda au kuonyesha vyeti vya kuthibitisha kwamba hawana virusi vya Corona.Hata hivyo nchi saba bado zitasalia katka orodha hiyo.

Afrika Kusini, Brazil na Mexico zimeondolewa kutoka orodha hiyo , ambayo inahitaji wasafiri kujitenga katika hoteli iliyoidhinishwa kwa gharama yao kwa siku 10 .

Waziri wa Uchukuzi Grant Shapps alisema mabadiliko yanaanza Jumatatu na ni " hatua inayofuata" katika kufungua safari za ndege.

Hatua hii ya hivi karibuni ni habari njema kwa sekta ya usafiri wa ndege na familia zilizotengwa wakati wa janga hilo.

Panama, Colombia, Venezuela, Peru, Ecuador, Haiti na Jamhuri ya Dominika wanabaki kwenye orodha hiyo

Nchi hizi pia zimeondolewa kutoka orodha hiyo inayowahitajin wasafiri kujitenga katika karantini kwa siku kumi ;

Afghanistan, Angola, Argentina, Bolivia, Botswana, Brazil, Burundi, Cape Verde, Chile, Congo (Democratic Republic), Costa Rica, Cuba. Eritrea, Eswatini, Ethiopia, French Guiana, Georgia, Guyana, Indonesia, Lesotho, Malawi, Mayotte, Mexico, Mongolia, Montenegro, Mozambique, Myanmar, Namibia, Nepal, Paraguay, Philippines, Réunion, Rwanda, Seychelles, Sierra Leone, Somalia, South Africa, Sudan, Suriname, Thailand, Trinidad and Tobago, Tunisia, Uruguay, Zambia na Zimbabwe.

Akitangaza mabadiliko ya hivi karibuni, Bwana Shapps alisema serikali "inafanya iwe rahisi kwa familia na wapendwa kuungana tena".

Alisema kuwa kwa vizuizi vichache "na watu wengi wanaosafiri, tunaweza wote kuendelea kusonga mbele kwa njia salama pamoja katika njia yetu ya kupona".

Mbali na orodha fupi ya nchi zenye zuio kusafiri bila ithibati ya vipimo vya Corona serikali ilisema abiria hivi karibuni wataweza kutumia picha ya kuthibitisha matokeo ya vipimo vyao vya corona kama sharti laj kuthibitisha kwamba wamepimwa na kupatikana bila ugonjwa huo .