Search This Blog
Saturday, October 2, 2021
Chanjeni acheni imani potofu kwenye usalama wa afya zenu
Na Maridhia Ngemela.
Wananchi wa Wilaya ya Kwimba kata ya Maligisu mkoa wa Mwanza wamepatiwa elimu ya umuhimu wa chanjo ya uviko 19 ilikuendelea kujikinga na janga hilo.
Zoezi hilo la elimu limefanyika leo katika Mkoa wa Mwanza wilaya ya Kwimba hii ikiwa ni muendelezo wa kuwapatia wananchi uwelewa juu ya ugonjwa huo na umuhimu wa kuchanja ikiwa ni njia moja wapo ya kujikinga na maambukizi ya uviko 19.
Miongoni mwa wananchi waliopata chanjo ni Lucas machinga mkazi wa kijiji cha kadashi amesema kutokana na elimu aliyoipata kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza na Mganga mkuu wa chanjo ni salama na ninawashauri Watanzania ambao bado wanaimani potofu waache mara moja jitokezeni tuchanje ili tuwe salama amesema Machinga.
Pasikali Majinge ni miongoni mwa waliopata chanjo amesema kutokana na ushawishi wa mkuu wa mkoa nimeamka kuchanja ila pia mtoto wangu alikuwa anasisitiza sana tuchanje na kwavile huduma hii umefika nimeamka nichanje ili niendelee kuwa salama zaidi Mimi pamoja na familia yangu amesema Majinge.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Robert Gabriel amesema kuwa chanjo ni salama na wananchi wajifunze kufuatilia maelekezo yanayotolewa na wataalamu wa afya na waachane na imani potofu waangalie usalama wa afya zao.
" Elimu potofu zimekuwa tumepoteza wafanyakazi wetu kwa ugonjwa huu ni hatari tusidanganyike kwa sababu miruzi mingi humpoteza mbwa mwelekeo hivyo tuchanje ili kuokoa maisha na kuwa na afya bora " anaeleza Gabriel.
Pia amewaasa wananchi hao kutokwenda kwa waganga wa kienyeji kuhusiana na ugonjwa huo kwani hawatapata msaada wowote bali kinga bora ni kupata chanjo ya UVIKO -19.
Kwa upande wake Mwenyekiti Mwenza wa kamati ya amani Mkoa Charles Sekelwa na mjumbe wa kamati hiyo Mohammed Moledina ameelaza kuwa chanjo ni salama hivyo wananchi wajitokeze kuchanja ili kuleta amani na muungano wa kifamilia.
Waliongeza kuwa viongozi wa dini zote wanaumoja na ushirikiano katika kupambana na ugonjwa huo hivyo wananchi wachangamkie fursa hiyo ili kujenga afya na kuendelea kasi ya uchapaji kazii ili kujijenga kiuchumi nakukuza maendeleo binafsi na taifa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...
No comments:
Post a Comment