Korea Kaskazini imelilaumu Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, kwa undumilakuwili kufuatia mazoezi ya kijeshi katika mataifa wanachama wa Umoja huo.
Jo Chol Su, Mkurugenzi wa idara katika wizara ya mambo ya nje inayohusika na mashirika ya kigeni, amesema Baraza hilo limeendelea kunyamaza kuhusu Luteka ya kijeshi iliyoongozwa na Marekani pamoja na washirika wake iliyohusisha pia majaribio ya silaha.
Su, amesema kukutana kwa Baraza hilo kunamaanisha dharau ya wazi ya uhuru wa taifa hilo na ni dalili ya uchochezi.
Kulingana na shirika la habari la serikali, tamko hilo limetolewa wakati kukiwa na ukoasoaji wa kimataifa dhidi ya majaribio ya urushaji makombora kutoka Korea Kaskazini uliofanyika hivi karibuni.

No comments:
Post a Comment