Search This Blog

Sunday, October 3, 2021

Merkel na Steinmeier kuhudhuria sherehe za Muungano mjini Halle

 


Kansela wa Ujerumani Angela Merkel na rais Frank Walter Steinmeier, watakuwa miongoni mwa maafisa wakuu serikalini wanaohudhuria maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 31 ya muungano kati ya Ujerumani Magharibi na Iliyokuwa Ujerumani Mashariki mwaka 1990. 

Mwaka huu mji wa Halle katika jimbo la Saxony Anhalt ndio unaoandaa sherehe ya Muungano na kama ilivyokuwa mwaka uliopita sherehe hizo zinafanyika kwa kuhudhuriwa na watu wachache kutokana na janga la virusi vya corona. 

Wanasiasa wakuu Olaf Scholz wa chama cha SPD na Armin Laschet kutoka chama cha Merkel cha CDU pia watahudhuria sherehe hizo zinazokuja wiki moja baada ya kufanyika uchaguzi Ujerumani. 

Merkel anaemaliza muda wake anatarajiwa kutoa hotuba yake ya mwisho kama kansela. Kansela huyo wa Ujerumani ataondoka uongozini pale serikali mpya ya mseto itakapoundwa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...