Search This Blog

Wednesday, September 29, 2021

WHO yasikitishwa na unyanyasaji wa kingono DRC


Shirika la Afya Duniani, WHO limetoa ripoti inayoonesha kuwa wafanyakazi wa mashirika ya misaada waliwanyanyasa kingono wanawake kadhaa na wanaume wakati wa mripuko wa ugonjwa wa Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo. 
 
Ripoti hiyo imewasilishwa jana na tume huru ya uchunguzi iliyoteuliwa na WHO. Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema amesikitishwa na madai hayo yaliyofanywa kati ya mwaka 2018 na 2020 na ameomba radhi.
 
 Tume hiyo ilizungumza na wanawake 63 na wanaume 12 walioathiriwa. Madai hayo yalijulikana mwaka mmoja baada ya uchunguzi wa shirika la habari za masuala ya kibinaadamu na taasisi ya Thomson Reuters. 
 
Unyanyasaji huo haukufanywa tu na mashirika ya Umoja wa Mataifa kama vile WHO, la kuwahudumia Watoto, UNICEF na la Wahamiaji, IOM, lakini pia mashirika ya misaada kama vile Oxfam, madaktari wasio na mipaka, World Vision na ALIMA.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...