Search This Blog

Wednesday, September 29, 2021

Wabunge wa upinzani waliokamatwa Uganda baada ya kuachiwa kufikishwa mahakamani leo

Wabunge wawili walio na ufungamano na mwanasiasa wa upinzani wanatarajiwa kufikishwa mahakama leo kwa madai ya kupanga mashambulio mabaya katika mkoa wa Masaka kusini mashariki.

Muhammad Ssegirinya na Allan Sewanyana wa chama cha National Unity wamekanusha mashataka dhidi yao na kuishtumu serikali kwa kuwatesa.

Kulingana na kituo cha NTV Uganda, siku ya Jumanne wabunge wa upinzani walitoka nje ya bunge kulalamikia hatua ya vyombo vya usalama kuwakamata tena wabunge wenzao wawili ambao walikuwa wameachiliwa kwa dhamana.

Karibu watu 30 waliuawa kwa kukatwa mapanga na magenge ya uhalifu mjini Masaka katika shambulio lililoanza mwezi Julai.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...