Maafisa watano wa kijasusi wameuawa nchini Sudan na wapiganaji wanaodaiwa kuwa wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu. Maafisa wa Sudan wamesema shambulizi hilo lilitokea jana kwenye mji mkuu, Khartoum.
Taarifa ya Shirika la Ujasusi la Serikali, GIA imesema kuwa wanamgambo hao walivifyatulia risasi vikosi vya serikali wakati walipovamia maeneo wanakojificha katika eneo la Gabra kusini mwa Khartoum.
Shirika hilo limesema maafisa wake watano wameuawa na mmoja amejeruhiwa na kwamba wamewakamata wapiganaji 11 na wanaendelea kuwatafuta wengine waliofanikiwa kukimbia. Rais wa Sudan Abdalla Hamdok ametuma salamu za rambirambi kuomboleza vifo vya maafisa hao watano.
Shambulizi hilo limefanyika wiki moja baada ya vikosi vya serikali kusema vimezuia jaribio la mapinduzi ambalo limeongeza mvutano kati ya majenerali wa kijeshi na wajumbe wa kiraia katika serikali ya mpito.
No comments:
Post a Comment