Search This Blog

Thursday, September 9, 2021

Watu watatu wafariki dunia kwa ajali ya Bodaboda

Watu  3 wenye umri kati ya miaka 15 hadi 18 wanaoishi kitongoji cha Shagiro Tazegwa kata ya Itilo wilaya Ya Nzega Mkoani Tabora wamekufa papo kwa papo baada ya kugongana uso kwa uso na gari aina ya fuso wakati wakiwa wamebebana kwenye  usafiri wao wa pikipiki.

Akizungumza na vyomba vya habari jana kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Safia Jongo alisema kwamba ajali hiyo  imetokea september 7 mwaka huu majira ya saa 12 jioni katika eneo la Tazegwa katika barabara itokayo Nzega mjini kuelekea mkoani Tabora baada ya gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T 587 BCF Kugongana na pikipiki ambayo aikuwa na namba za usajili wa pikipiki.

Alisema kwamba  kuwa chanzo cha ajari hiyo ni madereva wa pikipiki walikuwa wanatoka nzega mjini na kuelekea katika kitongoji cha Shagiro na walipofika eneo hilo la Tazegwa waliziovateki gari mbili aina ya malori pasipo kuangalia vizuri na ndipo walipokutana uso kwa uso na fuso na kugogwa na kupoteza maisha pale pale.  

Kamanda huyo wa polisi aliendelea kusema kwamba  kuwa vijana hao watatu waliokuwa katika pikipiki hiyo  moja walikuwa mwendo wa kasi sana na ajari hiyo imetokana na kutokuwa na umakini pindi wanapokuwa barabarani.

Safia  aliwataja watu walifariki  katika ajali hiyo kuwa ni  Paulo Petro,Rubeni Jogi na mmoja akitambuliwa kwa jina la Nasoro.

Kamanda huyo wa Polisi mkoani Tabora aliendelea kusema kwamba  vijana hao walikufa hapo hapo kwa kugongana uso kwa uso na gari aina ya fuso ambalo nalo lilikuwa likiovateki maloii na kuvaana na vijana hao watatu waliokuwa na pikipiki ambao nao walikuwa wakiovateki maloli.

Mwenyekiti wa kitongoji  cha Shagiro Tazengwa Marko Kazwiru alisema chanzo cha ajari hiyi ni madereva kutokuwa makini wa pande zote mbili na kuwaomba madereva kuzingatia kanuni za barabarani pindi wanapotumia vyombo vya moto.

Diwani wa kata ya Itilo Paskar Kigalu akiizungumzia ajari hiyo  amekiri kutokea katika eneo lake na kutoa pole kwa familia hizo tatu zilizopoteza ndugu hao na kusema watashirikiana bega kwa bega katika msiba huo.

Miili ya vijana hao watatu imeifadhiwa katika hospitali ya halmashauri ya mji wa nzega kwa ajili ya hatua za mazishi baada ya jeshi la polisi wilayani hapa kufika katika eneo hilo la ajari kwa ajiri ya uchunguzi zaidi  .

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...