Na Edina Fidelis, Morogoro.
Mamlaka ya Bandari Tanzania TPA inatarajia kufanya mashindano ya michezo Bandari Interpots Games Mkoani Morogoro ambayo yatajumuisha taasisi hiyo pamoja na taasisi nyingine ambazo zitashiriki mashindano hayo yatakayofanyika Septemba 13 hadi 20 mwaka huu.
Michezo itakayofanyika ni pamoja na mpira wa miguu, pete, wavu, kuvuta kamba kwa wanawake na wanaume pamoja na michezo mingine mingi, huku mgeni rasmi katika ufunguzi wa michuano hiyo akitarajiwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Afisa mawasiliano na mjumbe wa kamati ya michezo TPA Bwana Focus Mauki wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa ambapo amesema kutakuwa na michezo mbalimbali ambayo itafanyika katika uwanja wa jamhuri na kiwanja cha mpira wa wavu cha JKT Bwalo La Umwema vilivyopo mjini Morogoro.
Aidha amesema timu zitakazoshiriki ni pamoja na timu ya Bandari kutoka, Bandari ya Dar es Salaam,Tanga, Mtwara, Zanzibar pamoja na timu zinazoundwa na mikoa ya maziwa mkuu.
Ameongza kuwa kutokana na maombi mengi kutoka kwa wadau wa michezo kutoka taasisi na sekta mbalimbali, mashindano ya mwaka huu yatashirikisha pia timu kutoka kitengo cha kontena kutoka bandari ya dar es salaam TISTS, shirika la huduma za meli.
Hata hivyo amesema kuwa mamlaka ya bandari Tanzania TPA imetoa timu tano huku kukiwa na timu nyingine ambazo tayari zitashiriki kutokana na mashindano hayo kuwa na muamko mkubwa kila mwaka.
Kwa upande wao wajumbe wa kamati ya maandalizi ya michezo TPA akiwemo mwenyekiti wa wafanyakazi kutoka Bandari ya Dar es salaam Mashaka Karume na Priscilla Mkoka wamewataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa jamuhuri kushuhudia michezo mbalimbali hasa kwa upande wa wanawake.

No comments:
Post a Comment