Raia nchini Ujerumani wanapiga kura leo kulichagua bunge jipya, ambalo litatoa muongozo wa nani ataekirithi kiti cha Kansela Angela Merkel baada ya miaka 16 ya kuliongoza taifa lenye uchumi mkubwa kabisa barani Ulaya.
Mnyukano mkali katika uchaguzi huu unahusisha kambi ya kihafidhina ya Kansela Merkel, inayohusisha vyama vya ndugu vya CDU/CSU, ambavyo mgombea wao ni Arimin Laschet na yule wa chama cha Social Democrats-SPD, Olaf Scholz.
Takribani watu milioni 60.4 kati ya raia jumla milioni 83 wa Ujerumani ndio wenye uwezo wa kupiga kura kulichagua bunge, ambalo litakuwa na mamlaka ya kuchagua kiongozi mpya wa serikali.

No comments:
Post a Comment