Search This Blog

Sunday, September 26, 2021

Wananchi Zanzibar watakiwa kuunga mkono juhudi za Rais Mwinyi

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Khamis Hamza Chilo ambae ni Mbunge wa Jimbo la Uzini amewataka wananchi wa Zanzibar kuunga mkono juhudi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapimduzi  Dkt. Husein Ali Mwinyi za kuwaweka Wazanzibari kuwa wamoja ili kufikia maendeleo ya Uchumi wa Buluu.

Ametoa kauli hiyo huko Machui Jimbo la Uzini wakati akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi na  Jumuiya zake katika kikao cha kutathmini shughuli za kimaendeleo zilizofanywa na Viongozi wa Jimbo hilo.


Amesema  ili kufikia maendeleo ya Uchumi wa Buluu Zanzibar ni vyema wazanzibari kuungana  pamoja bila ya kujali tofauti zao za kisiasa, dini na kuulinda umoja na mshikamano uliokuwepo tokea kufanyika kwa Mapindunzi ya Zanzibar na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Aidha amewahimiza viongozi hao kuwa waadilifu na kupanga mipango madhubuti itakayosaidia kukipa ushindi Chama Cha Mapinduzi katika  chaguzi zake za ndani zinazotarajiwa kufanyika mwaka 2022 na kuchagua Viongozi waliyobora kwa uchaguzi wa mwaka 2025 kutoka ndani ya Chama hicho.

Akizungumzia maendeleo yaliyoletwa na viongozi wa Jimbo hilo ni pamoja na kusambaza umeme katika Kijiji cha Kiboje na Bambi Kijibwe Mtu, kusambaza mipira ya maji, kuchimba Visima, kujenga minara na kueka matenki ya kuhifadhia  maji kwa vijiji viliyokuwa vinakosa huduma hiyo  muhimu .

 


Nae Mwakilishi wa Jimbo hilo Haji Shaaban Waziri  amesema viongozi wa Jimbo hilo wamekusudia kuondosha changamoto ya uhaba wa vyumba vya madarasa kwa kujenga madarasa mapya na kufanya ukarabati kwa baadhi ya Skuli zinazovuja ili kusaidia wanafunzi kupata Elimu iliyobora .

Akitaja Skuli ambazo zimejengwa na zipo hatua ya mwisho kukamilika ni pamoja  na Skuli ya  Msingi Mchangani, Ujenzi wa vyumba sita vya madarasa, Skuli ya Bambi Msingi, Vyumba vinane vya kusomea na Skuli ya Msingi Koani, vyumba sita vya madarasa na ukumbi wa kufanyia Mitihani katika Skuli ya Msingi Kidimni.

Aidha ameeleza kuwa  Viongozi wa Jimbo hilo kwa kusaidiana na wafadhili mbali mbali wa maendeleo wanatarajia kujenga kiwanja cha Michezo katika Kijiji cha Bambi kitakachokuwa na uwezo wa kukusanya watu 10000 kwa wakati mmoja sambamba na nyumba watakazofikia wanamichezo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...