Kiasi wapiganaji 50 wa kundi la waasi wa Houthi na wanajeshi wa serikali nchini Yemen wameuwawa katika wakati mapigano yanaongezeka kuwania udhibiti wa jimbo la Marib lenye utajiri wa mafuta.
Duru za kijeshi kutoka upande wa serikali zimesema katika muda wa saa 48 zilizopita, wapiganaji 43 wa kundi la waasi wa Houthi wameuwawa na wengi wao ni kutokana na mashambulizi ya anga yaliyofanywa na muungano wa kijeashi unaongozwa na Saudi Arabia.
Inaarifiwa kuwa mamia ya watu wameuwawa ndani ya mwezi Septemba pekee baada ya waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran kuanzisha tena mashambulizi katika jimbo la Marib ambalo ndiyo ngome ya mwisho ya serikali ya Yemen inayoungwa mkono kimataifa.
Tangu mwezi Februari waasi hao wamezidisha juhudi za kulikamata jimbo hilo wakitumai ushindi utaimarisha nafasi yao katika mazungumzo ya kusaka amani.

No comments:
Post a Comment