Wagombea watatu wa nafasi ya ukansela nchini Ujerumani leo watachuana kwenye mdahalo wa mwisho wa televisheni wiki moja kabla ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Septemba 26.
Armin Laschet, mgombea wa vyama ndugu vya kihafidhina vya CDU/CSU, atapambana ili kumpiku mgombea wa chama cha SPD, Olaf Scholz, anayeongoza kwenye kura za maoni ya umma.
Uchunguzi wa maoni ya umma unaonesha kwamba SPD inaongoza kwa alama kadhaa, mbele ya muungano wa vyama vya CDU/CSU wa Kansela Angela Merkel huku chama cha Walinzi wa Mazingira kikishika nafasi ya tatu.
Mdahalo huo utakaorushwa na vituo vya televisheni vya ARD na ZDF utawapambanisha Laschet, Scholz na mgombea wa ukansela kwa tiketi ya chama cha Walinzi wa Mazingira, Annalena Baerbock.

No comments:
Post a Comment