Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Jamii imeshauriwa kuendelea kujitoa katika kuwasaidia watoto wenye ugonjwa wa Usonji ili watimize ndoto zao na kuachana na imani potofu.
Hayo yamesemwa leo hii Mkoani Mwanza katika zoezi la mbio za rock city marathon ambazo zimewakutasnisha watoto wenye ugonjwa wa Usonji na watu wazima zikiwa na lengo la kuwachangia fedha za kuwajengea kituo cha kuwalelea watoto hao na kupata matibabu kutokana na huduma wanazozihigaji.
Waziri mkuu mstaafu Mizengo Pinda alipokuwa akizindua mbio hizo amesema kuwa,anawafahamu wagonjwa wenye maradhi mbalimbali ila hajawahi kukisimia.
"Amesema ninawafahamu walemavu mbalimbali na ninaishi nao baadhi yao ila hawa viumbe wa Mwenyezimungu wenye ugonjwa wa akili nilikuwa sikijui mwalimu wangu ni huyu mama amenielimisha vya kutosha nikamwambia bibi nitakuja nikamuuliza unakadiris kuna watoto wangapi wenye ugonjwa huu anasema takribani watoto mia moja kwahiyo tendo hili ni la Mungu sisi ambao tuko wazima Mungu anataka tujitoe zaidi kuwasimamia hivyo mmefanya jambo la utu sana amesema Pinda.
Naye mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala aliyezungumzia kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa mwanza amesema kuwa lengo la mbio hizo ilikuwa kukusanya fedha zakuwasaidia watoto wenye tatizo la Usonji ila pia ni njia moja wapo ya kufanya mazoezi kuweza kujiepusha na maradhi mbalimbali.
Masala amesema kimsingi leo tumepata nafasi ya kukimbia kulikuwa aina tatu za kukimbia kulikuwa na kilometa 3za watoto ,kilometa 8 na kilometa17 na Mimi nimefanikisha kukimbia kilometa 17 lengo la mbio hizi ilikuwa ni kuhamasisha jamii kutambua ugonjwa wa Usonji na kuchangia kuweza kutatua tatizo hili na kilele cha mbio hizi itakuwa leo jioni katika uzinduzi wa kitambu cha mtoto mwenye Usonji pale viwanja vya Rock city more kwawale watakao pata nafasi wajitokeze.
Mwenyekiti wa maafa na starehe wa Rock city runners Abdallah Magoma alipokuwa akisoma risala amesema miongoni mwa changamoto walizozibaini ni watoto wenye ugonjwa wa Usonji na uhaba wa wataalamu wa ugonjwa huo na wazazi wenye watoto hao kufuata matibabu mbali na kwa gharama kubwa hali inayopelekea kunyanyapaliwa na jamii kwa kushindwa kupata huduma na kumudu gharama za matibabu kwani ziko juu lakini pia kusababisha baadhi ya wazazi kukimbia familia na kuweka imani potofu juu ya watoto hao.
Magoma amesema Usonji ni tatizo la mfumo wa fahamu linalopelekea kushindwa kuwasiliana kuzoea mazingira mapya ni tatizo ambalo halijapewa kipaumbele kama matatizo mengine mkoa wa Mwanza unawatoto wenye Usonji takribani miamoja ila miongoni mwao wanaopata matibabu ni watoto 30 kutokana na matibabu yao kuwa ya gharama kubwa na wengi wao hawana bima za afya hivyo tunaomba michango yenu ambayo itaweza kujenga kituo cha kuwalelea kitakacho gharimu shilingi milioni mia tano za Kitanzania.



No comments:
Post a Comment