Search This Blog

Sunday, September 19, 2021

Australia yapinga madai ya Ufaransa juu ya mkataba wa kununua nyambizi

Waziri Mkuu wa Australia Scott Morrison leo ameyapinga madai ya Ufaransa kwamba serikali yake ilidanganya kuhusu mipango ya kuufuta mkataba wa kununua nyambizi za Ufaransa, akisema tahadhari ilitolewa miezi kadhaa iliyopita. 

Morrison amesema kwa muda mrefu serikali mjini Canberra ilielezea wasiwasi wake kwamba nyambizi walizotaka kununua kutoka Ufaransa zisingekidhi viwango ambavyo Australia inavihitaji kwa ajili ya ulinzi wa kimkakati. 

Matamshi ya Morrison yanakuja baada ya waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa kuikosoa Australia kufuatia uamuzi wake wa kuingia mkataba mwingine wa kununua nyambizi zinazoendeshwa kwa nguvu ya nyuklia kutoka Marekani. 

Mkataba huo mpya kati ya Australia, Marekani na Uingereza umeikasirisha Ufaransa iliyosema kwamba imesalitiwa na kuchochea mvutano wa kidiplomasia baina ya mataifa hayo washirika.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...