Search This Blog

Sunday, September 26, 2021

Uingereza kutoa vibali vya muda kukabiliana na uhaba wa wafanyakazi

 


Uingereza itatoa vibali karibu 10,000 vya muda kwa madereva wa malori ili kupunguza upungufu mkubwa wa wafanyakazi. 

Tangazo la vibali vya muda vitakavyodumu hadi mwezi Desemba, limetolewa wakati mawaziri wakipambana na upungufu wa madereva na wafanyakazi wengine muhimu, hali iliyoathiri usambazaji mafuta na viwanda vingine. 

Misururu mirefu ya magari imeshuhudiwa katika vituo vya mafuta nchini Uingereza, wakati raia wakipuuzia tangazo la serikali la kutoingiwa na hofu na kununua mafuta kwa pupa. Baadhi ya vituo vya mafuta vilifungwa kutokana na kukosekana mafuta. 

Serikali ya waziri mkuu Boris Johnson, imedhibiti sheria za uhamiaji ikidai kuwa utegemezi wa taifa hilo kwa wafanyakazi wa kigeni lazima umalizike. 

Uingereza inakabiliwa na upungufu wa takribani madereva 100,000 kutokana na wengi wao kuacha kazi, Brexit na janga la virusi yva corona.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...