Search This Blog

Sunday, September 26, 2021

Raia zaidi ya milioni 60 wa Ujerumani kushiriki uchaguzi wa leo

 


Zaidi ya raia milioni 60 wa Ujerumani, leo wanashiriki uchaguzi wa bunge na Ukansela. 

Mgombea wa Ukansela kupitia chama cha SPD Olaf Scholz hivi karibuni alikuwa mbele kidogo dhidi ya mgombea wa muungano wa kihafidhina Armin Laschet, kulingana na kura za maoni. 

Jumla ya vyama 47 na makundi, vinashiriki uchaguzi wa leo. 

Muungano wa vyama ndugu vya CDU/CSU, SPD, chama cha kijani, FDP, Chama mbadala kwa ujerumani AfD na kile cha kushoto Die Linke, huenda vikaingia katika bunge la 20 la Ujerumani Bundestag. 

Wakati vituo vya kupigia kura vitakapofungwa saa 12 jioni, utabiri wa kwanza wa matokeo utatolewa na utabiri mwingine utatolewa hapo baadae. 

Kansela Angela Merkel, ambaye ameliongoza taifa hilo lenye nguvu zaidi kiuchumi barani Ulaya kwa miaka 16, hagombei katika uchaguzi wa leo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...