Manchester United bado wanamsaka mlinzi wa RB Leipzig na Ufaransa Nordi Mukiele, mwenye umri wa miaka 23, kuwa kiungo wa safu ya nyuma-kulia wa klabu hiyo. (Fichajes - in Spanish)
Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner, 25, alitaka kujiunga na Manchester United kabla ya kuhamia Stamford Bridge. (Bild - in German)
Winga Mdenmark anayewindwa na Tottenham na Sampdoria mwenye umri wa miaka 21- Mikkel Damsgaard, pia anatafutwa na Juventus. (Tuttosport - in Italian)
Arsenal watalazimika kulipa takriban pauni milioni 38.5 iwapo watataka kusaini mkataba namshambuliaji Mmorocco Youssef En-Nesyri, 24. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Manchester City wanataka kusaini mkatba na mshambuliaji mwenye umri wa miaka 16 wa Westham anayechezea timu ya walio chini ya miaka 17 ya England Divin Mubama. (Football Insider)
Juventus wanaripotiwa kuwa watamuuza kiungo wa kati wa Wales Aaron Ramsey, 30 mwezi Januari - huku klabu za West Ham, Everton na Newcastle zikimtaka. (Sun)
Inter Milan zimemuweka mlinda lango wa Arsenal na Ujerumani Bernd Leno, 29 katika orodha ya wachezaji wanaowalenga kuwachukua . (Fichajes - in Spanish)
Tottenham wanangalia uwezekano wa kumnunua mshambuliaji wa kati Juventus na Sweden mwenye umri wa miaka 21 Dejan Kulusevski. (Mirror)
Chelsea wako tayari kumuuza kiungo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 30 N'Golo Kante msiumu ujao. (Fichajes - in Spanish)
Chelsea wanajiandaa kufanya dau jipya kwa ajili ya winga wa Italia Federico Chiesa. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23- yuka katika mkataba wa mkopo wenye kipengele cha kununuliwa katika Juventus kutoka Fiorentina. (Calciomercato - in Italian)
Mlinzi wa Leicester City na Uturuki Caglar Soyuncu, mwenye umri wa miaka 25, ni mmoja wa wachezaji wanaotafutwa na Real Madrid. (DefensaCentral - in Spanish)











No comments:
Post a Comment