Rais wa Urusi Vladmir Putin amesifu uchaguzi wa bunge uliofanyika wiki iliyopita akisema ulikuwa huru na wa haki.
Rais Putin ametoa kauli hiyo wakati wa mazungumzo na wanasiasa kutoka vyama vilivyo na uwakilishi katika bunge jipya la taifa Duma.
Chama cha United Russia kimeshinda uchaguzi huo kwa asilimia 49.8, wakati nafasi ya pili ikikamatwa na chama cha kikomunisti na asilimia 18.9 ya kura.
Mamia ya waandamanaji walikusanyika mjini Moscow jana Jumamosu kupinga matokeo hayo ya uchaguzi ambayo yamegubikwa na madai ya udanganyifu.
Upinzani unadai kwamba kulikuwa na udanganyifu wa kimfumo katika kura zilizopigwa kwa njia ya mtandao.
Maandamano hayo kwenye uwanja wa Puskhin yalivutia polisi wengi, na vizuizi. Mamlaka zilikuwa zimetoa onyo mapema dhidi ya kushiriki katika maandamano yasiyoruhusiwa.

No comments:
Post a Comment