Search This Blog

Thursday, September 16, 2021

Uchomaji moto ni changamoto kwa miundo mbinu ya umeme Lindi



Na Ahmad Mmow, Lindi. 

Imeelezwa kwamba miongoni mwa sababu za uharibifu wa miundombinu ya umeme mkoani Lindi ni   uchomaji moto mapori. 

Hayo yameelezwa leo na meneja wa mkoa wa Lindi, wa shirika la usambazaji umeme nchini(TANESCO), Mhandisi Kainda Museru alipozungumza na wana  habari katika ofisi ya shirika hilo iliyopo katika   manispaa ya Lindi. 

Mhandisi Museru alisema uchomaji moto mapori unasababisha kuunguza nguzo. Kitendo ambacho kinachangia umeme kukatika mara kwa mara kwa. 

Alisema nguzo nyingi niza miti. Kwahiyo mapori yanapoungua, nguzo hizo pia zinaungua na kuanguka. Huku akibainisha kwamba juhudi kubwa za kufyeka majani na nyasi zinaz zunguka nguzo  zinafanyika. Hata hivyo idadi ya vibarua hailingani na ukubwa wa tatizo. 

Katika kupata suluhisho la kudumu la changamoto hiyo Mhandisi Museru alisema ni kudhibiti uchomaji moto. Huku akiweka wazi kwamba kazi ya kudhibiti uchomaji  inahitaji nguvu na juhudi za pamoja baina ya serikali na wananchi. 

 " Kazi ya kudhibiti uchomaji moto haiwezi kufanikiwa iwapo wananchi hawatatoa ushirikiano na shirika kwa kuwafichua wanaofanya kitendo hicho. Na vyombo vya habari vinawajibu wa kusaidia kutoa elimu kuhusu madhara yanayotokanana uchomaji moto," alisema Mhandisi Museru. 

Alisema uharibifu wa miundo mbinu licha ya kuisababishia hasara serikali, lakini pia unasababisha hasara kwa wananchi. Kwani umeme unapokatika shughuli nyingi za kiuchumi na uzalishaji mali zinasimama. 

Hata hivyo mtaalamu huyo alisema kuna kazi kubwa inafanyika kupitia wataalamu wa shirika hilo ili kukabiliana na uharibifu wa miundombinu. Hasa nguzo. Kwani tayari kazi ya kusimika nguzo za zege imeanza. Huku akiweka wazi kwamba mkakati uliopo ni kuwa na nguzo za zege badala ya miti. 

Mbali na hayo ya uchomaji moto na mkakati wa shirika hilo kutumia  nguzo za zege badala ya miti, alisema limepanga kufikisha umeme kwenye vijiji vyote 196 ambavyo havijafikishiwa. 

Alisema vijiji hivyo 196 ambavyo vipo katika mkoa huu wa Lindi vitafikishiwa nishati hiyo kupitia Wakala wa umeme vijijini(REA) ndani ya miezi 18 kuanzia sasa, kupitia awamu ya tatu ya mzunguko wa REA. 

Kutokanana matarajio hayo ya kufikisha nishati hiyo katika vijiji hivyo, alitoa wito kwa wananchi wa vijiji hivyo wajiandae kupokea nishati hiyo kwa kufanya maandalizi ya mambo muhimu yanayohitajika kabla ya kufikishiwa.

 Aidha meneja huyo wa TANESCO mkoa wa Lindi alitoa wito kwa wananchi hao  wajipange kwa  kuweka mipango thabiti ya kulinda miundo mbinu ya nishati hiyo muhimu kwa maendeleo na uchumi. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...