Search This Blog

Thursday, September 16, 2021

Mkuu wa Wilaya Hassan Masala ametoa maagizo haya kwa watendaji


Na Maridhia Ngemela, Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amefanya kikao cha majumuisho ya ziara yake aliyotembelea kata 19 kwa lengo la kusikiliza kero za wananchi,kujitambulisha, kukagua miradi ya maendeleo na kusimamia ulinzi na usalama wa Wilaya.

Masala amesema kuwa, katika kata zote 19nilizotembelea nimekuta a na changamoto zifuatazo,migogoro ya ardhi,miundombinu mibovu,fidia kwa wananchi,upungufu wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya afya,ukosefu wa maji na umeme,kutosomwa mapato na matumizi na wananchi kufanya biashara kiholela hizi ni kero ambazo nimekuta a nazo katika ziara yangu nimezungumza na wahusika kuzitatua changamoto hizi kwa kuwashirikisha wananchi na kuwapatia elimu itakayosaidia kuzitatua amesema Masala.


"Ilitujenge madarasa,tumalize zahanati za mama na mtoto , miundombinu tunahitaji fedha,tunataka kukusanyamapato mapato haya yanatokea kwetu huko kwa watendaji wa kata ,wenyeviti tushuke chini tukusanye mapato kuna watu wanavyanzo vya mapato huko wamevikali Mkurugenzi fanta kazii tuko na wewe tutakula ulinzi watakuita sana chemba simamia mapato,ni aibu umeenda shule x unakuta maendeleo na shule nyingine hakuna na inatakiwa kuwapanga wamachinga tumepewa mwezi mmoja kwahiyo tufanye kazii kwa ushirikiano ili tufikie malengo haya ni maagizo ninayotoa huwa sipendi kutoa maagizo yapuuzwe amesema Masala.

Mkuu wa Wilaya amewaomba wenyeviti wa mitaa kuuliza maendeleo yanayofanyika katika mitaa yao kwani ni haki yao kuuliza ili waelezwe na wafanye vikao na wananchi kwa lengo la kuleta maendeo na siyo kuwaacha wananchi hawaelewi nini kinaendelea kutoka serikalini.


Naye Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angeline Mabula ameshauri katika sekta ya ardhi wananchi wanaodai fidia wawewavumilivu ili kuepusha migogoro ambayo inaweza kujitokeza na kusababisha usumbufu unaoweza kujitokeza.

Ilemela tumefanya vizuri katika kutoa hati kitaifa hivyo naomba wananchi wanaodai fidia wasirudishiwe maeneo yao hasa maeneo ya kujenga shule huu utaratibu wa kulipa kidogo kidogo utaendelea na kama mko tayali kulipa kwa soko la leo sidhani kama halmashauri itaweza kulipa na utaratibu uliouanza mh mkuu wa wilaya endelea nao wa haya makampuni ambayo tuliyapa dhamana kuwapimia wananchi wameshindwa warudishe fedha na wananchi msidanganye katika kuandikisha majina katika umiliki wa ardhi tutazipunja familia zetu na kuzinyima haki andikeni majina yaliyopo Nida itamsaidia sana Serikali kutambua wamiliki halali amesema Mbunge wa Jimbo la Ilemela Angeline Mabula alipokuwa akizungumza katika kikao hicho.

Kikao hicho cha majumuisho ya ziara limeudhuriwa na wakuu wa shule za msingi na sekondari,wenyeviti wa mitaa,madiwani na wakuu wa idara kwa lengo la kuweka mikakati ya kutatua changamoto alizozibaini Mkuu wa Wilaya Hassan Masala.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...