Search This Blog

Sunday, September 5, 2021

Tunaomba Serikali kututizama kwa jicho la huruma tunachangamoto shuleni

 

Na Maridhia Ngemela,  Mwanza.

Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Hassan Masala amewataka wanafunzi  kutambua umuhimu wa kuwepo shule ili waweze kusoma kwa bidii  na siyo kupoteza muda  utakao pelekea kupata daraja la nne, sifuri.

Wito huo ameutowa  alipokuwa akizungumza na wanafunzi wa shule ya wavulana ya Bwiru kwenye ziara yake ya kutembelea kata 19 za wilaya hiyo ambayo inalengo la kukagua miradi inayotekelezwa na serikali.

Alisema ni vema wanafunzi kuona umuhimu wa kujisomea mara kwa mara ili waweze kufanya vizuri kwenye mtihani yao na kutimiza ndoto zao za baadae.

Alisema kila wanafunzi anapaswa kumtii mwalimu kwa kufuata maelekezo anayopewa  kwa sababu chini ya usimamizi wap kwani kufanya hivyo kutapelekea kufanya vizuri kwenye mtihani yao ya mwisho.

"Someni kwa bidii huwezi kuwa mjanja wakati huo umuhimu wa uwepo wako hapa na ukija mtihani unavuna sifuri na unakuwa umepoteza muda bila mafanikio yoyote.

Alisema serikali imewekeza fedha nyingi katika shule zote kwa kutengeneza na kukarabati  madarasa

Alisema  changamoto ya madawati ipo katika baadhi ya shule za msingi na sekondari atahakikisha wanafanyia kazi ili waweze kutatua changamoto hiyo.

"Nimesikia mmesema maji yanakatika mara kwa mara nitaongea na mtu wa Mwauwasa ashughulikie  ili  yapatikane muda wote wanafunzi waweze kuyatumia na kujiepusha na maradhi mbalimbali ili wasome kwa bidii.

Kutokana na changamoto ya viti na bweni moja limekamilika lakini bado halijaezekwa  tutakaa na uongozi wa shule ili kuweka mikakati ya kumaliza jengo hilo",Masala.

Naye Elisa Makoye akizungimza kwa niaba ya wanafunzi alisema  shule hiyo inakabiliwa na  upungufu wa vitabu kwa madarasa yote na upungufu wa viti  katika kidato cha tano ni vema serikali kuangalia kwa jicho la karibu ili waweze kutatua changamoto hiyo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...