Na Maridhia Ngemela, Mwanza.
Viongozi wa kuchaguliwa wameshauriwa kutoingilia majukumu ya watendaji wa Serikali katika ziara zao za kutimiza wajibu wao kwani imekuwa ikifedhehesha baadhi ya watumishi wa umma.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Zebedayo Selemani alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake kuwa imekuwa kero kubwa kwa watendaji wa Serikali kukosa amani na uwajibikaji wao kutoka kwa baadhi ya viongozi wa siasa kuwafedhehesha mbele ya wananchi na kuleta athari kwa jamii inayoishi nao kuwachukulia ni wakosefu wa nidhamu katika utendaji kazi wao.
"Amesema imefikia mahali sasa wao ndio wamekuwa mahakimu,takukuru ,askari kwenye mikutano ya hadhara akiangalia kitu anasema umeiba,wenye mamlaka ya kukamata ni polisi tena kwa maelekezo yenye staha hii maana njia wanazotumia viongozi wa siasa unaweza ikaleta athari kuchonganisha jamii na mtendaji wa serikali lazima tutumie vyombo husika nashauri tutumie vyombo ili vifanye kazi zao maana sasa Hawa watafanya kazi gani ?"amesema Zebedayo.
Ameishauri jamii kuendelea kufuata kwanini za afya ili kuendelea kujikinga na ugonjwa wa uviko 19 na kuweza kupata kinga ya chaji ambayo ni salama kwa Watanzani.

No comments:
Post a Comment