Search This Blog

Thursday, September 16, 2021

Tetesi za soka Kimataifa


Barcelona ina matumaini ya kumsajili kiungo wa kati wa Ufaransa na Man United Paul Pogba katika uhamisho wa bila malipo msimu ujao iwapo mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ataamua kutotia saini kandarasi mpya na Man United , ijapokuwa watakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka klabu za PSG , Juventus na Real Madrid . (Fichajes - in Spanish)

Mshambuliaji wa Chelsea na Ujerumani Timo Werner ,25, ni miongoni mwa wachezaji wanne wanaonyatiwa na Borussia Dortmund iwapo mshambuliaji matata wa klabu hiyo Erling Braut Halaand ataondoka katika klabu hiyo msimu ujao.(SportBild - in German)

Kandarasi ya beki wa Ujerumani Antonio Rudiger katika klabu ya Chelsea inakamilika msimu ujao na mazungumzo ya kuiongeza yamegonga mwamba. (Times - subscription required)Mkufunzi wa Arsenal Mikel Arteta anatarajiwa kumkuza kiungo wa kati wa timu ya wachezaji chipukizi katika klabu hiyo Charlie Patino katika kikosi cha kwanza cha timu hiyo huku kukiwa na ripoti kwamba klabu ya Barcelona inamnyatia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 17 wa England.. (Mirror)

 

Mmiliki wa klabu ya Fiorentina Rocco Commisso hajui iwapo mshambuliaji wa Serbia mwenye umri wa miaka 21 Dusan Vlahovic , ambaye amehusishwa na klabu ya Manchester City , Atletico Madrid na Juventus , ataongeza mkataba wake zaidi ya mwezi juni 2023 na klabu hiyo ya Itali. (Calciomercato, via Goal)

Naibu mkufunzi wa Newcastle Graeme Jones na mshambuliaji wa England Dwight Gayle, 30, walirushiana maneno makali katika uwanja wa mazoezi huku nahodha Jamaal Lascelles akilazimika kuingilia kati na kuwatawanya wawili hao. (Mail)

Mkufunzi wa Everton Rafael Benitez amepatia kipaumbele kumsajili beki wa kati katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.. (Football Insider)

Baadhi ya wanachama wa bodi ya klabu ya Barcelona wamemtaka rais wa klabu hiyo Joan Laporta kumfuta kazi mkufunzi Ronald Koeman baada ya kulazwa 3-0 na Bayern nyumbani.. (AS - in Spanish)

Tottenham ina hamu ya kumsajili mchezaji wa Borussia Monchengladbach Matthias Ginter lakini inakabiliwa na ushindani kutoka kwa Bayern Munich na Real Madrid ili kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 raia wa Ujerumani. (Calciomercato - Italian)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...