Ras Nicolas Maduro wa Venezuela jana, Ijumaa amewasili nchini Mexico, kwa ajili ya kushiriki mkutano wa viongozi wa Amerika ya Kusini na Karibiani, katika kile kinachoonekana kama safari ya nadra ya nje na ya kwanza tangu Marekani imtuhumu kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Kwa mujibu wa Twitter ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Mexico, Maduro alipokolewa na waziri wa wizara hiyo, Marcelo Ebrard kwa ajili ya kuhudhuria mkutano huo ambao utayashirikisha mataifa takribani 33.
Mkutano huo wa kilele ambao utafunguliwa na Rais wa Mexico, Andres Manuel Lopez Obrador, unatarajiwa kujadili athari za virusi vya corona katika ukanda huo. Obrado, kiongozi mwenye itikadi za mrego wa shoto ameonekana kuwa na uhusiano mzuri na Venezuela tangu aingie madarakani 2018.
Na 2019 serikali yake iligoma kumtambua mpizani wa Madulo, Juan Guaido pale alipojitangaza kuwa rais wa Venezuela.

No comments:
Post a Comment