Search This Blog

Saturday, September 18, 2021

ECOWAS: Rais Conde anaendelea vizuri baada ya kupinduliwa


Jumuiya ya Mataifa ya Ushirkiano wa Kiuchumi ya Afrika Magharibi, ECOWAS leo hii imesema rais aliyepinduliwa wa Guinea, Alpha Conde, ambae amewekwa kizuizini tangu mapinduzi dhidi yake mapema mwezi huu anaendelea vyema.
 
Katika tangazo lake hilo ECOWAS imesema ujumbe wake umefanikiwa kumuona Conde jana, Ijumaa, mjini Conakry, akiwa katika kizuizi cha nyumbani katika hoteli moja ya kifahari.Hiyo ni taarifa ya kwanza kabisa huru kuhusu hali ya rais, tangu kupinduliwa kwake Septemba 5.
 
 Ujumbe wa ECOWAS ambao unawajumuisha Rais wa Ghana Nana Akufo Addo, Rais wa Ivory Coast Alassane Outtara, vilevile wamekutana na kiongozi wa kijeshi, Mamady Doumbouya.
 
Taarifa imesema mazungumzo yao yalikuwa ya wazi na kirafiki, na kwamba wana imani ya kupatikana suluhisho. 
 
Lakini siku moja kabla, ECOWAS walitangaza marufuku ya kusafiri, vikwazo vya kibiashara dhidi ya waongoza mapinduzi na familia zao pamoja na kutoa miezi sita ya taifa hilo kufanikisha uchaguzi.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...