Vietnam imeidhinisha matumizi ya chanjo iliyotengenezwa nchini Cuba iitwayo Abdala, kwa ajili ya matumizi dhidi ya aina mpya ya virusi vya corona katika kipindi hiki ambacho taifa hilo linakabiliana na kiwango kibaya zaidi cha mripuko wa virusi hivyo.Abdala inakuwa chanjo ya nane ya Covid-19 kuidhinishwa katika nchi hiyo yenye viwango vidogo zaidi vya kutoa chanjo kwa watu wake katika eneo la Kusini/mashariki mwa Asia.
Asilimia 6.8 tu, kati ya watu wake milioni 98 ndio waliokamilishwa kuchanjwa mara mbili.Tangazo hilo lilitolewa katika kipindi cha takribani masaa machache, baada ya rais wa Vietnam, Nguyen Xuan Phuc kuondoka mjini Hanoi kwenda Havana, Cuba kwa safari ya kikazi.
Vietnam imerekodi visa vya maambukizi ya virusi vya corona zaidi ya 667,000 na vifo Takribani 17,000, ikiwa idadi kubwa ya vifo hivyo tangu Aprili vimetokana zaidi na aina mpya ya kirusi cha Delta.

No comments:
Post a Comment