Search This Blog

Saturday, September 4, 2021

Rais Bukele wa El Salvodor apewa idhini ya kugombea tena


Mahakama ya juu ya El Salvador imempa idhini rais Nayib Bukele kuwania muhula wa pili, licha ya katiba kumzuia mkuu wa nchi kutumikia mihula miwili mfululizo mamlakani. 
 
Uamuzi huo wa jana utamruhusu Bukele kugombea muhula wa pili mnamo mwaka 2024, na hivyo kumfanya kuwa rais wa kwanza katika taifa hilo la Amerika ya Kati kutumikia zaidi ya miaka mitano madarakani tangu miaka ya 1950. 
 
Uamuzi huo ulitolewa na majaji ambao waliteuliwa na Bukele mwezi Mei, baada ya bunge kuwaondoa majaji kadhaa ambao walikuwa wakosoaji wa serikali.
 
 Hatua hiyo ilielezewa kuwa ni mapinduzi na kuchochea miito ya ukosoaji kutoka jumuiya ya kimataifa. 
 
Bukele aliyechaguliwa mwaka 2019, ana uungwaji mkono mkubwa nchini El Salvador kutokana na ahadi za kupambana na uhalifu na kuimarisha usalama.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...