Search This Blog

Saturday, September 4, 2021

Afghanistan: Hatma ya bonde la Panjshir Valley mashakani huku mapigano makali yakiendelea


Hatma ya bonde la Afghanstan- eneo ambalo bado halijatwaliwa na Taliban - iko mashakani huku mapigano makali yakiendelea katika bonde hilo.

Vyanzo vya Taliban vimeliambia Shirika la habari la Reuters kwamba walikuwa wameliteka eneo hilo, lakini wapiganaji wapinzani wanaopigana nao walipinga taarifa hizi.

Mmoja wa viongozi wa makundi ya upinzani , Amrullah Saleh, alipuuzilia mbali madai kwamba alitoroka, lakini akasema hali ni "ngumu".

Mapigano katika bonde la Panjshiryanaripotiwa kuwauwa mamia ya watu.

katika mji mkuu Kabul na miji mingine watu kadhaa waliuawa na wengine wakajeruhiwa kutokana na ufyatuaji risasi uliofanywa kwa ajili ya kusherehekea a, taarifa zimesema.

Bonde la Panjshir , lililopo kaskazini mwa Mji mkuu Kabul, ni moja ya majimbo madogo zaidi ya Afghanstan ambayo bado hajachukuliwa na Taliban.

Bonde hili ambalo ni ngome ya jadi ya wanaopinga kipindi cha mpito cha ni makao ya watu kati ya 150,000 na 200,000 na ni eneo lililijificha nyuma ya vilele vya milima.

Upinzani - ambao unajumuisha vikosi vya zamani vya Afhanistan wna wanamgambo wa eneo hilo-unaongozwa na kiongozi wa kikabila wa eneo hilo Ahmad Massoud. Baba yake alifanikiwa kupigana na Wasovieti waliovamia miaka 1980 , na Taliban katika miaka ya 1990.

katika ujumbe wa video uliotumwa kwa BBC, Bw Saleh, makamu wa zamani wa rais wa Afghanistan, salisema kulikwa na majeruhi pande zote.

"Bila shaka tuka katika hali ngumu. Tunakabiliwa na uvamizi wa Taliban'' alisema ,"

Lakini aliongeza kuwa : "Hatutasalimu amri, tutasimama Afghanistan."

Alisema kuwa anashirikisha vido ili kuwahakikishia watu kwamba ripoti zinazosema kuwa ametoroka ni za uongo. Hatahivyo BBC haikuweza kupata thibitisho huru kuhusu eneo hili

1px transparent line

Ali Nazari, ambaye ni msemaji wa wapiganaji wa National Resistance Front (NRF) faliiambia BBC kwamba waasi walikuwa wamewarudisha nyuma Taliban.

"Kuna mamia ya Wataliban ambao wamemekwama. Na wanakimbia mapigano na kuna masharti ya mazungumzo yanayowataka wasalimu amri sasa hivi ," alisema.

Lakini maafisa wa Taliban wamekuwa wakidai ushindi wa eneo hilo, ambapo kamanda mmoja aliliambia shirika la habari la Reuters : " Kwa neema za Mungu muweza wa yote, tunaidhibiti Afghanistan yote. Wasumbufu wameshindwa na Panjshir sasa iko chini yetu ."

Taliban sasa wanadhibiti maeneo mengine yaliyobakia ya nchi, na wanatarajiwa kutangaza serikali mpya katika siku zijazo.

Muungano wa Ulaya na Uingereza Ijumaa walijiunga na Marekani, wakisema kuwa watakabiliana na kikundi hicho cha Kiislamu, lakini hawatawatambua kama Tkama serikali ya Afghanistan.

muungani wa Ulaya pia ulisema kuwa unapanga kufufua upya uwepo wake wa kidiplomasia mjini Kabul ili kusimamia uokoaji wa wa watu na kuhakikisha kwamba serikali mpya ya Afghanistan inatimiza ahadi zake kuhusu masuala mbali mbali, ikiwa ni pamoja na usalama na haki za kibinadamu.

Lakini waziri wake wa mambo ya nje Josep Borrell alisema kuwa mazungumzo yoyote yatatakiwa kuwa na masharti makali na yatakuwa juu ya kuwasaidia watu wa Afghanistan.

Mwandishi wa BBC wa masuala ya kimataifa Lyse Doucet, ambaye yuko Kabul, anasema kwamba huku Taliban ikitaka kukubalika kimataifa, wanataka hilo kwa kuzingatia masharti yao wenyewe.

Kama nchi za magharibi hazitaki kushirikiana nao kuna nchi nyingine zenye nguvu duniani kama vile Uchina , Urusi na Pakistan ambazo wanaweza kushirikiana nazo, aliongeza mwandishi wetu.

Wakati guo huo, taliban inasemekana kutoa amri kali dhidi ya ufyatuaji wa makombora ya anga baada ya taarifa ambao hazijathibitishwa za idadi ya vifo vilivyosababishwa na ufyatuaji risasi wa sherehe mjini Kabul na maeneo mengine ya nchi.

Mwnaume mmoja - Muafghanistan mwenye haki ya kuishi nchini Uingereza ambaye amekwama mjini Kabul , ameiambia BBC kuwa wakati ufyatuaji wa risasi ulipoanza Ijumaa usiku, "kila mtu alikuwa anakimbia kila upande, sawa manthari ya filamu".

Alisema kuwa alikuwa anatembea hadi miguu yake ikahisi ganzi , "nilifikiria haya yalikuwa ni matembezi yangu ya mwisho ya maisha".

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...