Search This Blog

Saturday, September 4, 2021

Waziri Mkuu wa Thailand anusurika kura ya kutokuwa na imani

Waziri Mkuu wa Thailand Prayuth Chan-ocha na mawaziri wengine watano wamenusurika kura ya bunge ya kutokuwa na imani nao leo Jumamosi wakati wanaharakati wakipanga maandamano zaidi dhidi ya serikali. Prayuth amepata kura 264 za kumuunga mkono dhidi ya 208 za hapana.
 
 Upinzani ulihitaji kura 242 kati ya kura 482 bungeni za kumwondoa waziri mkuu. Wabunge nchini Thailand kwa siku ya nne mfullizo wameituhumu serikali kwa kushughulikia vibaya janga la virusi vya corona na kumkosoa waziri mkuu Prayuth kwa athari mbaya za kiuchumi.
 
 Malalamiko mengine yanahusu kasi ndogo ya chanjo ya corona wanayodai inatokana na uagizaji mdogo wa chanjo hizo. Hii ni mara ya tatu kwa serikali kunusurika kuondolewa madarakani na inatokea wakati maandamano ya kuunga mkono demokrasia yakipangwa kufanyika leo Jumamosi.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...