Search This Blog

Tuesday, September 14, 2021

Putin anaidhinisha nyongeza ya mshahara kabla ya uchaguzi kwa polisi, wanajeshi

 


Rais Vladimir Putin leo hii ameidhinisha nyongeza ya mishahara kwa polisi na jeshi kabla ya uchaguzi wa bunge, moja ya hatua ambazo wakosoaji wanasema zinafanywa kwa lengo la kukisaidia chama tawala.


Katika amri yake iliyochapishwa katika tovuti ya ikulu ya Kremlin, Putin amesema mishahara ya wanajeshi na polisi itafanyiwa marekebisho kwa tarakimu za juu kuliko mfumuko wa bei katika miaka ya 2022 na 2023.


Kwa mwezi uliopita mfumuko wa bei nchini Urusi ulisimama katika asilimia 6.7, kiwango ambacho kimeonekana kuwa cha juu zaidi ya lengo la asilimia 4 la benki kuu ya taifa hilo.Chama tawala cha United Russia kinatarajiwa kushinda uchaguzi huo pamoja na kupungua kwa umaarifu wake na kuporomoka kwa viwango vya maisha nchini humo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...