Waziri wa Mambo ya Nje ya Ujerumani Heiko Maas amesema anataka kuongeza misaada zaidi kwa watu wenye kuhitaji nchini Afghanistan.
Akizungumza katika mkutano wa mataifa wahisani waziri huyo amesema Ujerumani tayari imeongeza kiasi cha euro milioni 100.Hata hivyo amesema upo mpango wa kuongeza Euro milioni 500 kwa lengo la kuuinga mgono Afghanistan na mataifa jirani.
Wakati huo huo ameutolewa wito utalawa mpya wa Afghanistan kutoa hakikisho la usalama wa kuingia misaada ya kibinaadamu.Aidha waziri huyo wa mambo ya nje wa Ujerumani amesema mbali ya misaada ya kiutu, mtazamo wao wa baadae kwa serikali ya Taliban si kutegemea kusikia maneno yao tu bali matendo yao.

No comments:
Post a Comment